 |
Ufundi wa ushonaji chuoni TUSIMA |
Taasisi ya Utafiti wa Waswahili ya Mashariki mwa Africa - TUSIMA ina vyuo mashuhuri vya ufundi wa Waswahili - Mombasa na Lamu ambazo huwawezesha vijana kutukuwa masomo ya ufundi yenye kiwango cha shahada. Masomo yenyewe ni kuwafundisha wanafunzi kutema mbao wakifunzwa nakshi za kibajuni, kigujarati, kiomani n.k, pia humuwezesha mwanafunzi kujuwa useremala kamili. Kwa upande wa kike, wanafunzi hufunzwa kushona nguo za kila mapambo, kutia darizi, kutia vito kofia za Kiswahili n.k. Kuna wale wanafunzi wakushinda kutwa na pia kuna wa koto(part-time). Kila mwaka TUSIMA hutowa matangazo kupitia vyombo mbali mbali vya habari kwa kujiandikisha kwa kozi zetu. Na mahitaji nikama ifuatayo:
 |
Barishiti na forona zilizotiwa darizi |
- Awe ni raia wa Kenya na mwenye umri wa kati ya 16 mpaka 25
- Awe amemaliza kuwango cha elimu ya shule ya msingi ama zaidi
- Kosi inategemea uwezo wa fahamu ya mtu ni kutoka mwaka moja hadi miwili
Mipango kabambe inaandaliwa kukifanya chuo kuwa na uwezo wakusajili wanafunzi wa shahada ya Diploma kupitia ya ushirika wa vyuo vengine vikuu vya elimu humu nchini. Kosi hizi ziliundwa sikwaajili kuhuhisha turathi za Kiswahili peke bali pia ni kuhifadhi na kulinda mila na desturi za wa Waswahili wasehemu zote za miji ya kale hadi mji mkongwe Zanzibar
 |
Kazi za mbao chuoni TUSIMA |
No comments:
Post a Comment