Maonyesho ya Soko Tembezi katika Village Market Nairobi ni hatuwa muhimu katika kuleta biashara ya vitu pamoja na huduma mbali mbali katika makusanyiko mamoja. Soko hili liliazimiya kuwapa fursa muhimu wahudumu wa sekta ya utalii nafasi ya kufanya biashara na ulimwengu wote. TUSIMA ilishiriki miongoni mwa washirika wengine 55 na kila mmoja alionyesha vitu vyake huku akitumainiya wateja kununua bidha hizo.
Maonesho ya vyombo vya Kiswahili katika soko tembezi Village Market Nairobi |
Lengo la kushiriki kwa RISSEA ilikuwa ni kupanua fikra za kibiashara na kugundua masoko mapya. Hivo basi, tulianika vyombo maridadi vya Kiswahili na kazi ashiki za darizi ili kupata wateja na huku tukijifunza kutoka kwa wenzetu.
Kuwahudumiya kikamilifu wateja wetu ndilo lengo na shabaha yetu. Bidhaa zetu zinapatikana katika Makumbusho ya Nairobi na katika afisi zetu za TUSIMA Mombasa na Lamu.
No comments:
Post a Comment