Tuesday, August 31, 2010

SHEREHE YA KUSHUWA JARIDI LA KWANZA LA TUSIMA

Wageni mashuhuri waliohudhuri tamasha za ushwuaji wa jarida
Mnamo terehe 24 Aprili 2010, TUSIMA ilichanja mbuga mpya katika maendeleo ya shirika la Makumbusho ya Kitaifa ya Kenya kushuwa jarida lake la mwanzo hapo Ngome ya Yesu Mombasa mgeni mheshimiwa akiwa ni Bwana Issa Timami ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Makumbusho ya Kitaifa ya Kenya. Jarida hili liliwezeshwa kwa ufadhili wa kampuni ya Fairdeak Holdings. Miongoni mwa waliohudhuriaya ni pamoja na mkurugenzi Mkuu wa MKK Daktari Idle Farah Omar , Profesa Mohamed Abdulaziz, Washauri wa TUSIMA, Bwana Hussein Zakir Mkurugenzi wa fairdeal, Bwana Mahmoud Noor wa SEACOM na wengineo. Mbali na jarida hilo TUIMA iliweza piya kushuwa tovuti yake mpya www.rissea.org ambayo ilitengezwa upya kwa msaada wa SEACOM, kampuni ya Just Imaging na Kenay Data Network.

Kaimu Mkurugenzi wa TUSIMA alitowa nasaha kuwa jarida hili jipya litakuwa silakuelimisha jamii pekee kuhusu ratiba na taratibu za TUSIMA bali litakuwa chomba muhimu kuwaunganisha jamii, wasomi na watafiti mbali mbali kutuma nakala kumbatana na mipango ya TUSIMA
Wageni waalikwa wakilipitia jarida jipya la TUSIMA


SANAA NA UFUNDI WA WASWAHILI

Ufundi wa ushonaji chuoni TUSIMA
Taasisi ya Utafiti wa Waswahili ya Mashariki mwa Africa - TUSIMA ina vyuo mashuhuri  vya  ufundi wa Waswahili - Mombasa na Lamu ambazo huwawezesha vijana kutukuwa masomo ya ufundi yenye kiwango cha shahada. Masomo yenyewe ni kuwafundisha wanafunzi kutema mbao wakifunzwa nakshi za kibajuni, kigujarati, kiomani n.k, pia humuwezesha mwanafunzi kujuwa useremala kamili. Kwa upande wa kike, wanafunzi hufunzwa kushona nguo za kila mapambo, kutia darizi, kutia vito kofia za Kiswahili n.k. Kuna wale wanafunzi wakushinda kutwa na pia kuna wa koto(part-time). Kila mwaka TUSIMA hutowa matangazo kupitia vyombo mbali mbali vya habari kwa kujiandikisha kwa kozi zetu. Na mahitaji nikama ifuatayo:
Barishiti na forona zilizotiwa darizi

  • Awe ni raia wa Kenya na mwenye umri wa kati ya 16 mpaka 25
  • Awe amemaliza kuwango cha elimu ya shule ya msingi ama zaidi
  • Kosi inategemea uwezo wa fahamu ya mtu ni kutoka mwaka moja hadi miwili
Mipango kabambe inaandaliwa kukifanya chuo kuwa na uwezo wakusajili wanafunzi wa shahada ya Diploma kupitia ya ushirika wa vyuo vengine vikuu vya elimu humu nchini. Kosi hizi ziliundwa sikwaajili kuhuhisha turathi za Kiswahili peke bali pia ni kuhifadhi na kulinda mila na desturi za wa Waswahili wasehemu zote za miji ya kale hadi mji mkongwe Zanzibar
Kazi za mbao chuoni TUSIMA

JAMII YA MALINIDI WAPOKEYA TAMASHA LA KWANZA LA KITAMADUNI LA MALINDI KWA SHANGWE

Ngoma za kitamaduni za kimijikenda
Tamasha la kwanza la Malindi lilikuwa la siku tatu kuanziya tarehe Pili hadi Nne ya Aprili 2010. Waandalizi wa tamasha hili walitoka Makumbusho ya Kitaifa ya Kenya wakiwamo wa TUSIMA na wakiwamo washidau kutoka Malindi na MADCA.

Tamasha hili litakuwa likiandawa kila mwaka kwa shabaha ya kuhuisha turathi za kitamaduni ambazo zinapoteya kwa haraka sana kutokana na athari za kigeni. Pia ni fursa kubwa kuzileta pamoja jamii zote zinazoishi Malindi ilikuonesha turathi tafauti na pia kuendeleza amali zoa zinazohusiana na turathi.

Shamra shamra nyingi zilikuwako wakati wa tamsha hili ikiwamo moenesho ya vakula va asili, ngoma za kienyeji, sanaa za kiasili, michezo kwa vijana na mashindano ya mashua, uvuvi na upakaji wa hina.Pia kuliandaliwa warsha iliyosimamiwa na kuongoza na TUSIMA 

Bali na hayo wanawake hawakuwacha nyuma siku hiyo walionyesha ngoma mbali mbali za wanawake kama lelemama na vugo. Pia walisaidiya kuwavisha kiasili wasichana katika maonesho ya kujitanda leso. 
Goma kutoka Malindi

Tamasha zenyewe zilisambazwa katika maeneo kadha ya Malindi moja wapo ni Jengo lazamani la Ofisa wa Taarafa ambapo maonesho ya sana za kiasili zilitandikwa hapo na pia maenyesho ya leso tofauti tofauti zilizodhaminiwa na mwana biashara maarafu wa leso Bwana Abdalla Leso. Na kiwanja cha mpira kilioka mbele ya makumbusho ya Malindi. Sehemu hii kila aina za ngoma za kienyeji zilioneshwa na kuwatumbuiza wageni.


Mashindano ya uvuvi wakati wa tamasha

MAONESHO YA SOKO TEMBEZI LA 2010

Maonyesho ya Soko Tembezi katika Village Market Nairobi ni hatuwa muhimu katika kuleta biashara ya vitu pamoja na huduma mbali mbali katika makusanyiko mamoja. Soko hili liliazimiya kuwapa fursa muhimu wahudumu wa sekta ya utalii nafasi ya kufanya biashara na ulimwengu wote. TUSIMA ilishiriki miongoni mwa washirika wengine 55 na kila mmoja alionyesha vitu vyake huku akitumainiya wateja kununua bidha hizo.

Maonesho ya vyombo vya Kiswahili katika soko tembezi Village Market Nairobi
Lengo la kushiriki kwa RISSEA ilikuwa ni  kupanua fikra za kibiashara na kugundua masoko mapya. Hivo basi, tulianika vyombo maridadi vya Kiswahili na kazi ashiki za darizi ili kupata wateja na huku tukijifunza kutoka kwa wenzetu.

Kuwahudumiya kikamilifu wateja wetu ndilo lengo na shabaha yetu. Bidhaa zetu zinapatikana katika Makumbusho ya Nairobi na katika afisi zetu za TUSIMA Mombasa na Lamu.