Thursday, September 16, 2010

TUSIMA YAWAPIKU MAHARUSI KATIKA UKUMBI WA AGA KHAN

Bwana Harusi akiwa na vazi la joho
TUSIMA ilijibwaga katika ukumbi wa Aga Khan mjini Mambasa wakati wa Idd Ul Fitr na kuonesha mapambo ainati ya maharusi wa Kiswahili.

Maonesho haya yaliyoandaliwa na wachapishaji wa jarida la EVE yaliazimiya kuwaleta wapambaji pamoja na washonaji wa nguo na mapambo mengine ya maharusi kuonesha bidha hizo ili wapate kujulikana na kujenga uhusiano na wateja wapya. Maonesho haya yalifanyika kuanziya tarehe 10 hadi 12 Septemba 2010.

TUSIMA ilionesha mavazi ya bwana na bibi harusi wa Kiswahili yakiwamo majoho, magauni, vibeti, mikoba, marinda na bidhaa nyinginezo za maharusi. Wageni wengi walitembeleya maandalizi ya TUSIMA na kupendezewa nayo. Wawakilishi wa TUSIMA walijijulisha kwa wateja wengi wapya ambao walifurahiya bidhaa hizo. Wawakilishi hawa walitiwa moyo sana na maonesho haya hata wakahamasika kufanya yao au kushiriki tena katika maonesho kama haya mwakani.

Wednesday, September 15, 2010

MWITO WA IKHTISARI WAKOMA

Jumba la ofisi kuu ya RISSEA
Kadhiya ya mwito wa ikhtisari kwa kongamano la kimataifa la RISSEA litakalofanyika hapo Novemba mwaka huu umekoma. Jumla ya ikhtisari 25 zilipitishwa na Kamati ya Urejelezi na waliyofaulu tayari wameshajulishwa kutayarisha makala zao kamili. Mawanda yaliyogusiwa kuligana na ikhtisari hizo ni pamoja na ilimu insi, isimu, historiya, fasihi, dini na uchumi wa ardhi. Makala kamili yanatarajiwa mnamo tarehe 8 mwezi wa Novemba mwaka huu.

Thursday, September 2, 2010

ISTILAHI ZA KISWAHILI

ISTILAHI       KISAWE      UFAFANUZI

Global       Zingiro           Global kwa Kiswahili itawakilishwa na zingiro kwa sababu 
                                      ni kitu mviringo au duwara.

Scanner    Tambazo        Tambazo kuwakiliswa na scanner lina maana kutaza au 
                                     kueneza.

Internet     Ungamano      Ungamano lina maana internet kuunganiisha au 
                                      kuwaunganisha watu mbali mbali  kuweza kusikilizana.
                                    
Office    Ukurungwani     Ukurungwani lina maana ya office,mkurungwa ni officer 
                                    neno la zamani la Kiswahili

Radio      Mwengoya      Mwengoya lina maana ya radio kutokana na neno mwengo 
                                    kwa kiengereza ni echo utanda kazi wake ni sauti ya kuja 
                                    kutoka mbali uliko wewe maana mwengo wa 
                                    kuya = mwengoya.

Computer  Ngamizi    Computer linawakilishwa na neno ngamizi kwa ajili ya utenda 
                                kazi  wake maana nikupokeya ukitiacho cha meza ikiwa ni 
                                vitabu ni maandishi anajaza bila ya kukataa ile iharibike.

Mouse   Kitauzi        Mouse linawakilishwa na kitauzi maana kifaa chenya 
                                kuchagua unachotakakukiona kukivuta kije mbele yako 
                                katika ngamiza

Fax      Pepesi        Fax linawakilishwa neno la Kiswahili pepesi lina maana 
                              ya mfano wakupepesa utenda kazi wake.

E-mail   Baruwa pepe E-mail linawakilishwa na baruwa pepe yaani baruwa yenye
                                kupeperushwa kwa njia ya Kiamu pepe ni umeme.

Ray        Uka         Ray linawakilishwa na uka katika matumizi ya kumepambauka
                             kwa lahaja ya Kiamu, kwa kisanifu kumepambazuka kwa wingi
                             ni nyuka.

Picture  Uyoo          Picture linawakilishwa na uyoo kutokana na kuiyowa.


Science  Ulimbe       Science linawakilishwa na ulimbe lenya maana ya elimu
                               ya ulimwengu na viumbe.

Psychology Ushunuzi  Psychology linawakilishwa na ushunuzi lenya maana
                                  ya kushuwa yaliyomo ndani kudhihirika nje.


No: Prof. Ahmed Sheikh Nabahany
Swahili consultant
TUSIMA